Sendiga aitaka Babati mji kutafuta ufumbuzi wa taka
11 April 2024, 6:16 pm
Halmashauri ya mji wa Babati yatakiwa kutafuta magari ya kuzolea taka.
Na Angel Munuo
Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga ameitaka Halmashauri ya mji wa Babati kuhakikisha wanatafuta ufumbuzi wa kupata magari ya kuzolea taka wakati wakijipanga kupata gari kubwa la kuzolea taka.
Sendiga ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwepo kwa taka nyingi katika maeneo ya mji wa Babati na kutokuzolewa kwa wakati katika majalala ya kuhifadhia taka hali ambayo amesema ni hatari kwa afya za wananchi
Awali wananchi na wafanyabiashara waliopo karibu na jalala lililopo karibu na uwanja wa Tanzanite kwaraa wilayani Babati mkoani Manyara walililamika kutoka na harufu mbaya inayotoka katika jalala hilo na kuiomba serekali kuzoa taka hizo au kuliondoa jalala hilo.