NHIF yaboreha kitita cha mafao
9 April 2024, 2:47 pm
Jamii mkoani Manyara imetakiwa kujiunga na mfuko Taifa wa bima ya Afya.
Na George Agustino
Jamii mkoani Manyara imetakiwa kujiunga na mfuko wa Taifa wa bima ya afya NHIF ili kuepuka gharama kubwa za matibabu wanapokwenda kupata huduma za matibabu katika hospital.
Meneja wa mfuko wataifa wa bima ya afya mkoa wa Manyara Joyce Sumbwe ameyasema hayo wakati akizungumza na Fm Manyara katika kipindii cha Mseto wa leo kuhusu kitita chaboreshwa mafao kilicho ndani ya mfuko huo, amesema ni utaratibu wa mfuko huo kuboresha huduma zao ili kuendana na Teknolojia nakusaidia kuondoa changamoto mbalimbali wakati wa utoaji wa huduma za Afya kwa mnufaika.
Aidha amesema hakuna gharama za ziada ambazo mnufaika wa mfuko wa bima ya Afya anatakiwa kulipa na ikitokea amedaiwa fedha anapokwenda kupata matibabu anatakiwa kutoa taarifa kwa kupiga simu namba ya huduma kwa wateja ambayo ni 199 ili kupatiwa msaada au kufika katika ofisi zao zilipo nchini nzima.