Wagonjwa 10 wa kipindupindu waruhusiwa Mrara
8 March 2024, 11:03 am
Wagonjwa waliokuwa wanaugua ugonjwa wa kipindu pindu waruhusiwa baada ya kupatiwa matibabu.
Na Mzidalifa zaid
Wagonjwa 10 waliokuwa wanaugua ugonjwa wa kipindupindu katika hospitali ya mji mrara wilayani babati mkoani manyara wameruhusiwa baada ya kupatiwa matibabu ambapo wananchi wametakiwa kuendelea kuchukua taadhari ya kujikinga na ugonjwa huo kwa kuwa na vyoo bora.
hayo yamebainishwa na Afisa afya Halimashauri ya mji wa babati Emanuel Kimonge alipokuwa akiongea na fm manyara, amesema hatua ambazo zimechukuliwa na halimashauri ni pamoja na kuwazuia mama lishe na baba lishe kupika vyakula pembezoni mwa barabara.
kwa upande wake mratibu wa elimu ya afya kwa jamii Halimashauri ya mji wa Babati Laurencia Urio amesema ugonjwa huo unaenea kutokana na uchafu ambapo wananachi wanatakiwa kuhakikisha wananawa mikono mara kwa mara. amesema njia nyingine ya kuepukana na ugonjwa huo ni kula chakula cha moto , kufunika chakula, kuosha matunda kabla ya kuyatumia, kuzoa taka zinazozunguka maeneo ya nyumbani, na wanaendelea kutoa elimu hiyo kupitia maeneo mbalimbali yenye mikusanyiko pamoja na katika vyombo vya habari.