Huheso FM

zima moto wajipanga kukabiliana na majanga ya moto

January 21, 2022, 12:12 pm

Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga, Hanafi Mkilindi, amesema jeshi hilo limejipanga kikamilifu katika kukabiliana na majanga yatakayotokea kipindi hiki cha mvua..

Akizungumza ofisini kwake leo amesema kwa kushirikiana na wananchi watafanikiwa katika kukabiliana na athari mbalimbali huku akiwataka wananchi kutoa taarifa mapema kwa ajili ya uokoaji.

Pia afisa huyo amewaomba wananchi wanaoishi katika sehemu za mabondeni kuhama na kwenda sehemu ambazo ni salama kwa kipindi hiki cha mvua.

Sauti ya mkuu wa jeshi la zima moto na uokoaji Wilaya ya Kahama

Hata hivyo amesema jeshi hilo limekuwa na kawaida ya kufanya ukaguzi wa miundombinu ya kuzimia moto kwenye maeneo ya makazi ya wananchi.