Huheso FM

Watakaofichua taarifa za ukatili wa kijinsia kulindwa

May 25, 2021, 7:25 pm

Imeelezwa vitendo vya rushwa katika jamii imekuwa miongoni mwa sababu inayochangia vitendo vya ukatili wa kijinsia kuendelea kutokea katika jamii na kupelekea waathirika wa matukio hayo kukosa haki.

Mratibu Taifa wa mtandao wa Utetezi wa haki za Binadam- THRDC Onesmo Olengurumwa amewaambiwa waandishi wa habari leo katika ofisi za shirika la HUHESO FOUNDATION lililopo mjini Kahama mkoani Shinyanga.

Katika hatua nyingine mratibu huyo wa THRDC amewasihi waandishi wa habari kuendelea kutoa elimu katika jamii na kuibua matukio ya ukatili wa kijinsia ili yaweze kushughulikiwa ikiwemo wahanga kupata haki yao ya msingi inayostahili kisheria.

Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika la HUHESO FOUNDATION,  Juma Mwesigwa mbali na kupongeza hatua hiyo ya THRDC kuwatembelea lakini pia ameahidi kuendelea kushirikiana na wadau katika kukabiliana na matukio ya ukatili wa kijinsia.