Huheso FM

Mchinjaji wa Nguruwe akamatwa na TAKUKURU Manispaa ya Kahama

April 21, 2021, 5:08 pm

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) wilayani Kahama imebaini uchinjaji wa mifugo kiholela ikiwemo iliyokufa hali ambayo inahatarisha afya za watumiaji wa nyama ambazo zinauzwa bila kufanyiwa uchunguzi na maafisa mifugo.

Mkuu wa TAKUKURU, Abdallah Urari amesema walipokea malalamiko ya wananchi kuhusiana na taratibu za uchinjaji na ilibainika kuwepo kwa eneo la machinjio ya Nyama za Nguruwe Mtaa wa Nyakato ambalo baada ya kujiridhisha iliagizwa kufukiwa.

Hata hivyo taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU imeitaka ofisi ya mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama kufunga machinjio yote ya kienyeji na kuweka utaratibu maalum wa uchinjaji wa Nguruwe utakaoweza kufuatwa na kudhibiti upotevu wa mapato.

MWISHO