FM Manyara
FM Manyara
10 April 2026, 18:07

Kuelekea maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto anayeishi na kufanya kazi mtaani , wananchi mkoani Manyara wametakiwa kutoa ushirikiano katika mapambano ya watoto waishio mtaani na kufanya kazi mtaani.
Na Mzidalfa Zaid
Wito huo umetolewa leo na afisa ustawi wa jamii mkoa wa Manyara Khadija Muwango wakati akiongea na fm Manyara, amesema siku ya mtoto anayeishi na kufanya kazi mtaani huadhimishwa april 12 kila mwaka .
Aidha, amesema mkoa wa Manyara utaadhimisha siku hii kwa kutoa elimu katika halmashauri zote za mkoa wa Manyara ambapo amesema kuna sababu mbalimbali zinazopelekea kuwepo kwa tatizo hilo ikiwemo changamoto za kifamilia.