FM Manyara
FM Manyara
9 April 2026, 17:57

Wananchi mkoani Manyara wameshauriwa kujitokeza katika kambi maalum ya matibabu na upasuaji katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Manyara kuanzia april 19 hadi april 24 mwaka huu itakayohusisha madaktari bingwa na wataalamu bobezi kutoka marekani.
Na Mzidalfa Zaid
Ushauri huo umetolewa leo na daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake na afya ya uzazi kutoka hospital ya rufaa mkoa wa Manyara Michael Haule , wakati akiongea na fm Manyara radio amesema kutakuwa na matibabu mbali mbali ikiwemo upasuaji maalum( plastic surgery ) kurekebisha makovu yaliyotokana na ajali au moto, matibabu ya mdomo sungura,upasuaji wa jumla, huduma za pua, sikio, koo, macho ,matibabu ya mifupa, matibabu ya magonjwa ya wanawake na uzazi pamoja na uchunguzi wa saratani.

Kwa upande wake daktari bingwa wa pua,masikio na koo kutoka hospitali ya rufaa mkoa wa Manyara Athanas Budodi, amewataka wananchi wote wenye changamoto za pua masikio na koo kufika hosptalini hapo kupatiwa matibabu.
Nae daktari wa kitengo cha macho kutoka hospitali ya rufaa mkoa wa Manyara Mathias Kimaro, amesema katika kambi hiyo kutafanyika huduma za macho ambapo amewataka wananchi wote wenye tatizo la macho yanayosumbua kuhudhuria katika kambi hiyo.
