FM Manyara

Polisi Babati wapatiwa elimu ya nishati safi ya kupikia

3 April 2026, 12:26

Picha ya maafisa kutoka Shirika la Tanesco na maaskari wa jeshi la polisi

Maafisa  wa jeshi  la  polisi  wilayani  Babati mkoani Manyara wamepatiwa elimu  ya  matumizi ya nishati safi ya kupikia  kwa kutumia  majiko ya kisasa yanayotumia umeme, ikiwa ni juhudi  za serikali  kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kuendelea kulinda  mazingira.

Na Emmy Peter

Elimu hiyo imetolewa  na  afisa uhusiano  kwa umma  Tanesco  mkoa wa Manyara, Samwel Mandari katika ukumbi wa Polisi messi uliopo Babati, ambapo, amesema matumizi ya majiko ya umeme ni  nafuu, yanaokoa  muda na gharama, pamoja  na kuwa salama kwa mtumiaji.

Mandari amesema majiko  hayo  ya kisasa aina ya pressure cooker  kutoka  kwa wakala Sescom, yamethibitishwa na kampuni ya Sescom, yana uwezo wa kuandaa chakula kwa muda mfupi, na kusaidia kuongeza ufanisi katika matumizi ya nishati.

sauti ya afisa uhusiano  kwa umma  Tanesco  mkoa wa Manyara, Samwel Mandari

Aidha,amesema maafisa hao wanapaswa kuwa mabalozi wa elimu hiyo kwa jamii, kwa kuwa matumizi ya nishati safi ni sehemu ya mkakati wa serikali katika kulinda mazingi kwa jamii.