FM Manyara

Manyara wanufaika na kambi ya matibabu

3 April 2026, 10:44

picha ya baadhi ya wananchi ambao wamepatiwa huduma

Zaidi ya wananchi 2700 wamenufaika na kambi ya matibabu  ya afya  ya siku sita  iliyoratibiwa na shirika la SO THEY CAN Tanzania kwa kushirikiana  na halmashauri ya wilaya ya Babati mkoani Manyara.

Na Marino Kawishe

Akihitimisha  kambi  hiyo ya matibabu  ya  afya  iliyofanyika  kwenye  kata nne  zinazofanya kazi na  shirika  la  STC mkuu wa chuo cha elimu  maalumu  Patandi, mwalimu Lucian Segesela amesema chuo hicho kitaendelea kutoa ushirikiano pamoja na vifaa vitakavyohitajika  ili kusaidia upatikanaji wa afua mbali mbali. 

sauti ya mkuu wa chuo cha elimu  maalumu  Patandi, mwalimu Lucian Segesela

Kwa upande wake meneja mkazi wa  shirika la  STC Roselyne Mariki amekiri kuwepo na mafanikio makubwa na kuahidi kuendelea kushirikiana na serikali ili kufanya kambi zaidi ambazo zimekuwa  msaada mkubwa kwa wananchi  wenye changamoto  za  kifedha .

sauti ya meneja mkazi wa  shirika la  STC Roselyne Mariki

Nae muuguzi mkuu wa hospital ya wilaya ya Babati sister Thea Funto ametoa wito kwa wananchi kuhudhuria hospital ili kupata matibabu na sio kusubiria kambi za afya ambazo hufanyika mara chache kwenye maeneo yao.

sauti ya muuguzi mkuu wa hospital ya wilaya ya Babati sister Thea Funto
Picha ya muuguzi mkuu wa hospital ya wilaya ya Babati sister Thea Funto

Aidha,kambi nyingine ya afya   imepangwa kufanyika kwenye  kata nne  za galapo, qash, endakiso na mamire mwanzoni mwa  mwezi september  ambapo  wananchi wameomba  kuongezwa kwa huduma ya x- ray ili kusaidia wenye uhitaji  kwenye eneo hilo.