FM Manyara

Wanawake Manyara washauriwa kulima kilimo ikolojia

1 April 2026, 18:43

Picha ya mratibu wa vituo vya taarifa na maarifa mkoa wa Manyara Clara Malle (kushoto), mwanakituo wa taarifa na maarifa Mamire  ambae pia ni diwani wa viti maalum wilaya ya Babati Sesilia Cosmas (katikat) mwenyekiti  wa kituo cha taarifa na maarifa Mamire Magreth Basso(kulia)

Wanawake mkoani manyara wametakiwa kulima kilimo cha ikolojia ambacho hakitumia gharama kubwa ili kumuinua mwanamke kiuchumi  na kuepelekea kufanya shuguli zake kwa urahisi.

Na Mzidalfa Zaid

Wito huo umetolewa na mratibu wa vituo vya taarifa na maarifa mkoa wa Manyara Clara Malle, wakati akiongea na fm Manyara  amesema kilimo ikolojia ni kilimo rahisi na cha kumrahisishia mwanamke kufanya shughuli zote kwa pamoja.

Sauti ya mratibu wa vituo vya taarifa na maarifa mkoa wa Manyara Clara Malle

Kwa upande wake mwanakituo wa taarifa na maarifa Mamire  ambae pia ni diwani wa viti maalum wilaya ya Babati Sesilia Cosmas amewataka wananchi kuwania nafasi mbalimbali za  za uongozi au maamuzi.

Sauti ya mwanakituo wa taarifa na maarifa Mamire  ambae pia ni diwani wa viti maalum wilaya ya Babati Sesilia Cosmas

Nae mwenyekiti  wa kituo cha taarifa na maarifa Mamire Magreth Basso, amesema kituo hicho kimekuwa kikipambana na ukatili wa kijinsia.

Sauti ya mwenyekiti  wa kituo cha taarifa na maarifa Mamire Magreth Basso