FM Manyara
FM Manyara
23 March 2026, 16:02

Leo ikiwa ni Siku ya Hali ya Hewa Duniani, wananchi mkoani Manyara wametakiwa kuzingatia ushauri unaotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) pamoja na kufuatilia utabiri unaotolewa.
Na Mzidalfa Zaid
Akiongea na FM Manyara mtabiri wa hali ya hewa mkoa wa Manyara Haji Hamimu amesema mkoa wa Manyara umeadhimisha siku ya utabiri wa hali ya hewa duniani kwa kutoa elimu kwa wananchi kupitia vyombo vya habari.
Aidha, amesema kauli mbiu ya hali ya hewa kwa mwaka 2026 ni pima hali ya hewa leo ili kesho iwe salama, ambapo amewataka wananchi kuzingatia utabiri unaotolewa kwa ajili ya usalama wao.