FM Manyara

Wenye mahitaji maalum Babati wapata viti mwendo

21 March 2026, 20:54

Picha ya viti mwendo vilivyotolewa na Taasisi ya Chem Chem, na Chair The Love kutoka Nchini Marekani

Taasisi ya Chem Chem na Chair The Love kutoka nchini Marekani kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Babati wamekabidhi viti mwendo zaidi ya 148 kwa wananchi wenye mahitaji maalum kutoka maeneo mbalimbali ya halmashauri hiyo.

Na Mwandishi Wetu

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi msaada huo kwa wananchi wenye uhitaji maalum, Meneja Mahusiano na Usimamizi wa Miradi ya Maendeleo ya Jamii kutoka Chem Chem Napendael Wazoel amesema lengo lao nikuisaidia jamii kupitia uhifadhi ambao umeendelea kuwanufaisha wananchi ambao wapo pembezoni mwa hifadhi.

Sauti ya Meneja Mahusiano na Usimamizi wa Miradi ya Maendeleo ya Jamii kutoka Chem Chem

Aidha akishukuru kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mwanasheria wa Halmashauri hiyo Jofrey Jaffar ameitaka jamii kuendelea kuunga mkono taasisi ambazo zimewekeza kwenye maeneo yao na ambazo zinaigusa jamii moja kwa moja kupitia misaada inayotolewa.

Sauti ya Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati

Nao wananchi wenye uhitaji maalum wameishukuru taasisi ya Chem Chem na washirika wake kwa msaada huo huku wakiomba taasisi hizo kuendelea kutoa msaada kwa wahitaji ambao bado hawajafikiwa kwa njia moja ama nyingine. 

Sauti ya wananchi wenye uhitaji maalum