FM Manyara

Wananchi 5000 wafanyiwa uchunguzi wa afya ya kinywa na meno Manyara

19/03/2026, 17:18

picha ya baadhi ya viongozi waliohudhuria katika maadhimisho ya wiki ya afya kinywa na meno

Zadi ya wananchi 5000 katika mkoa wa Manyara wamefanyiwa uchunguzi wa afya ya kinywa na meno ambapo Kati yao 318 wamepatiwa matibabu ya kuzibwa meno, 191 wamesafishwa, zaidi ya 500 wamen’golewa meno, 14 wamefanyiwa upasuaji mdogo, 3 upasuaji mkubwa  na 191 wamepatiwa seti za meno bandia.

Na Mzidalfa Zaid

Hayo yameelezwa Leo na Rais wa chama Cha wataalam wa afya Tanzania (TDA) DR Gemma Berege kinywa na meno Tanzania, katika kilele Cha maadhiimisho ya kitaifa ya siku ya afya ya kinywa na meno Duniani ambayo kitaifa yamefanyikia mkoani Manyara.

sauti ya Rais wa chama Cha wataalam wa afya ya Tanzania (TDA) DR Gemma Berege
picha ya Rais wa chama Cha wataalam wa afya ya Tanzania (TDA) DR Gemma Berege

Kwa upande wake mkurugenzi msaidizi wa huduma za kinywa na meno kutoka wizara ya afya Baraka Nzobo amesema asilimia 76 ya watanzania wameoza meno ambapo amesema changamoto hiyo inasababishwa na wananchi kutotumia dawa zenye viwango vinavyoendana na umri na kuwataka wataalam kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi sahihi ya mswaki.

sauti ya mkurugenzi msaidizi wa huduma za kinywa na meno kutoka wizara ya afya Baraka Nzobo

Katika maadhiimisho hayo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Babati Emmanuela kaganda ambae amemuwakilisha mkuu wa mkoa wa Manyara ambapo amekemea vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wananachi kwa kukata baadhi ya viungo kwenye kinywa na meno.

sauti ya mkuu wa wilaya ya Babati Emmanuela kaganda
picha ya mkuu wa wilaya ya Babati Emmanuela kaganda

Aidha, kauli mbiu ya wiki ya kinywa na meno mwaka 2026 ni :kinywa chenye furaha ni maisha yenye furaha ambapo wiki hii imeeadhimishwa kwa kutoa matibabu Bure ya kinywa na meno kwa wananchi pamoja na kuwapatia elimu.