FM Manyara

Vijana Manyara wahimizwa kujiajiri

19/03/2026, 16:58

Picha ya afisa biashara mkoa wa Manyara na Mkurugenzi wa Mgendi Minsupermarket na wadau mbalimbali

Vijana mkoani Manyara wamehimizwa kutoa fikra za kuajiriwa na kuweka mawazo yao katika kujiajiri ili kuweza kurithisha vizazi vyao katika biashara zao.

Na Diana Dionis

Hayo yamesemwa na Afisa biashara mkoani Manyara Ally Salehe Mokiwa katika uzinduzi wa Mgendi MinSupermarket yenye Biashara ya vitu mbalimbali vya nyumbani  ambapo amesema vijana waliojiajiri wanaweza kuwarithisha watoto wao biashara zao mbali na wale walioajiriwa

Sauti ya afisa biashara mkoa wa Manyara Ally Salehe Mokiwa

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mgendi Minsupermarket John Mgendi, amesema siri ya mafaniko ni kutokukata tamaa na kuwa na imani katika biashara, huku akiwasihi vijana kutokukata tamaa katika utafutaji wao wa kila siku.

Mkurugenzi wa Mgendi Minsupermarket John Mgendi