FM Manyara
FM Manyara
19/03/2026, 16:37

Picha ya mkuu wa TAKUKURU akikabidhi zwadi za eid kwa watoto wenye uhitaji
Jamii Mkoani Manyara, imetakiwa kuendelea kudumisha matendo mema baada ya mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani na mfungo wa kwaresma kama wanavyo fanya katika kipindi hiki.
Na Mzidalfa Zaid
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Babati, Emmanuela Mtatifikolo Kaganda, aliposhiriki Iftar maalumu iliyoandaliwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Manyara, na kuwakutanisha wadau mbalimbali.

Kwa upande wake mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Manyara Bahati Haule, amesema lengo la kuandaa iftar hiyo ni kuiweka TAKUKURU karibu na jamii huku akisema kuwa wametoa msaada kwa watoto yatima katika kituo Cha Hossana home care foundation ambao pia wameshiriki iftar hiyo.

Akiongea kwa niaba ya shekhe wa mkoa wa Manyara , Shekhe Ahamad Said ameishukuru TAKUKURU kwa kuandaa iftar hiyo na kuzitaka taasisi zingine kuiga mfano huo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa kituo Cha Hossana home care foundation Neema Munisi pamoja na watoto yatima wa kituo hicho wameishukuru TAKUKURU kwa msaada huo ambao wameutoa.