FM Manyara

Manyara kuwa mwenyeji wiki ya kinywa na meno-Matibabu kutolewa bure

10/03/2026, 16:58

picha ya msimamizi wa huduma za kinywa na meno  Pastor Mahendeka

Mkoa  wa  Manyara unatarajia  kuwa mwenyeji wa maadhimisho  ya wiki ya afya ya kinywa na meno duniani ,ambapo maadhimisho hayo yataadhimishwa kwa kutoa matibabu ya bila malipo ya  kinywa na meno kwa wananchi kuanzia  march 14 hadi march 18 mwaka huu.

Na Mzidalfa Zaid

Akiongea na fm Manyara msimamizi wa huduma za kinywa na meno  Pastory Mahendeka , amesema maadhimisho hayo yatakuwa na huduma mbali mbali ikiwemo elimu ya afya ya kinywa na meno, uchunguzi, matibabu  pamoja na mafunzo endelevu  kwa wataalamu………….

sauti ya msimamizi wa huduma za kinywa na meno  Pastor Mahendeka

Kwa upande wake daktari mfawidhi kutoka kitengo cha kinywa na meno hospital ya rufaa mkoa wa manyara Athuman Yatera amesema madaktari bingwa  kutoka  nchi nzima watakuwepo mkoani manyara ambapo amewataka wananchi wenye changamoto ya kinywa na meno kufika hospital ya mkoa au hospital ya halmashauri kupatiwa matibabu bure.

sauti ya daktari mfawidhi kutoka kitengo cha kinywa na meno hospital ya rufaa mkoa wa manyara Athuman Yatera
picha ya daktari mfawidhi kutoka kitengo cha kinywa na meno hospital ya rufaa mkoa wa manyara Athuman Yatera

Nae Mratibu wa kinywa na meno halmashauri ya mji wa Babati Catherine Cuthbert amesema matibabu hayo ya bila malipo yatajumuisha wagonjwa waliotoboka meno , changamoto ya fizi, mpangilio mbaya wa meno na changamoto yeyote ya kinywa na meno.

sauti ya Mratibu wa kinywa na meno halmashauri ya mji wa Babati Catherine Cuthbert
picha ya Mratibu wa kinywa na meno halmashauri ya mji wa Babati Catherine Cuthbert