FM Manyara
FM Manyara
05/03/2026, 18:03

Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kuchukua taadhari ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa covid 19 ambao uliripotiwa hivi karibuni katika baadhi ya maeneo hapa nchini.
Na Mzidalfa Zaid
Wito huo umetolewa na Mganga mkuu wa mkoa wa Manyara Andrew method , amesema katika kipindi hiki Cha mvua kumekuwa kukitokea magonjwa mengi hivyo wananchi wajilinde wasipate magonjwa hayo ambapo amesema katika mkoa wa Manyara Bado hakujaripotiwa kisa chochote.
Kwa upande wake afisa afya mkoa wa Manyara Switen Mwabulambo , amewataka wananchi mkoani Manyara kuzingatia taratibu zote za usafi mara kwa mara ili kuepuka ugonjwa huo.
