FM Manyara
FM Manyara
05/03/2026, 17:46

Katika kuelekea siku ya wanawake Duniani ,Wanawake wa halmashauri ya mji wa Babati mkoani Manyara wamepanda miti katika kituo Cha afya Sigino ili kuendelea kutunza mazingira.
Na Mzidalfa Zaid
Afisa maendeleo ambae pia ni mratibu wa dawati la mtambuka kutoka halmashauri ya mji wa Babati Ivetha Kaoga amesema kuelekea siku hiyo wamefanya matukio mbalimbali ya kijamii.
Kwa upande wake mganga mfawidhi wa kituo Cha afya Sigino Joseline Samwel pamoja na mwenyekiti wa kijiji Cha singu Fabian Kombe wamewashukuru wanawake hao kwa kupanda miti katika kituo hicho itakayosaidia wagonjwa kupata kivuli.
Mgeni rasmi katika zoezi hilo alikuwa ni mwenyekiti wa umoja wa wanawake wilaya ya Babati mjini Eva luoga amewataka Wanawake kuendelea kushirikiana katika masuala mbalimbali.

