FM Manyara
FM Manyara
04/03/2026, 16:47

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Manyara imefanikiwa kurejesha Shilingi milioni 15 za mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto yaliyokuwa hayajawasilishwa benki.
Na Mzidalfa Zaid
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake, kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Manyara Bahati Haule, amesema kwa kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2025 TAKUKURU kupitia ofisi yake ya Wilaya ya Kiteto ilifanya uchunguzi wa ukusanyaji wa mapato yatokanayo na ushuru wa mifugo minadani pamoja na tozo za Movement Permit katika biashara ya mauzo ya mifugo ikiwemo ng’ombe, mbuzi na kondoo.
Amesema baadhi ya watumishi walishindwa kuwasilisha fedha walizokusanya benki kwa wakati, huku wengine wakidaiwa kuzitumia kwa maslahi binafsi.
Aidha, amesema wamechukua hatua mbali mbali za kiutawala ikiwemo watumishi hao kusimamishwa kazi na kiasi kurejeshwa katika akaunti ya halmashauri.