FM Manyara
FM Manyara
04/03/2026, 16:33

Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amekabidhi Vyombo vya utoaji huduma ya maji ngazi ya jamii (SBWSO) vitakavyosaidia kurahishisha kufikisha huduma ya maji vijijini.
Na Mzidalfa Zaid
Akizungumza baada ya kukabidhi vyombo hivyo , Sendiga amesema ni jitihada za Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta Samia suluhu Hassan katika kufikisha huduma ya maji vijijini ambapo amewataka watumiaji wa vyombo hivyo kuhakikisha wanavitunza.

Kwa upande wake Meneja wa Ruwasa mkoa wa Manyara James Kionaumela amesema hali ya upatikanaji wa maji katika mkoa wa Manyara ni asilimia 78.09 Hadi December 2025.

Baadhi ya watumiaji vyombo hivyo ambao wamekabidhiwa pikipiki, wamesema zitawarahisisha kuyafikia maeneno mengi kwa wakati na kuhakikisha huduma ya maji inapatikana kwa wakati.
