FM Manyara
FM Manyara
28 February 2026, 6:32 pm

Wahitimu 13 wa elimu ya ngazi ya juu katika Chuo Cha East Africa Theological bible institute (ECLEA) kinachopatikana wilayani Babati mkoani Manyara wamehitimu mafunzo yao katika Chuo hicho wakiwa wamendaliwa kumtumikia Mungu katika jamii.
Na Mzidalfa Zaid
Akizungumza katika mahafali hayo mgeni rasmi wa hafla hiyo Askofu John Kazimoto amewataka wahitimu hao kufanya kwa vitendo yale yote waliyofundishwa huku wakiwa mabalozi wa kukitangaza chuo hicho kinachotoa elimu ya kimungu ikiwemo biblia
Kwa upande wake Mkuu wa chuo Cha East Africa Theological bible institute (ECLEA)Ibrahim Joram amewataka wahitimu hao kumtumikia Mungu siku zote na kuwa mfano wa kuigwa Katika jamii.
Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi, mwakilishi wa wahitimu Neema Silvester amesema wamepata mafanikio makubwa ikiwemo tafsri za kibibilia, msaada na upatanishi, uongozi Bora katika kanisa pamoja ndoa na malezi ya kimungu.