FM Manyara
FM Manyara
26 February 2026, 6:06 pm

Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta Mwigulu Nchemba amemuagiza Mkuu wa Takukuru mkoa wa Manyara kufuatilia fedha zilizotumika katika ujenzi wa jengo la halmashauri ya wilaya ya kiteto na ofsiis ya mkuu wa wilaya hiyo kabla ya kukamilika kwa ziara yake mkoani Manyara
Na Mzidalfa Zaid
Nchemba amesema hayo wilayani kiteto mkoani Manyara katika ziara yake ya kwanza baada ya kuzindua jengo la ofisi ya mkuu wa wilaya ya kiteto, amesema amepata taarifa za watumishi ambao walifanya ubadhirifu wa fedha za ujenzi wa jengo hilo , ambapo amempongeza mkuu wa mkoa wa Manyara kwa kufuatilia na kuzirudisha mapema fedha hizo na kutoa maagizo kuwa wahusika wote wachukuliwe hatua Kali za kisheria.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga, amesema kwa kipindi Cha awamu ya sita, mkoa wa Manyara umepokea Zaidi ya shilingi bilioni 700 ambapo amemshukuru kiongozi huyo kwa kuanza ziara yake mkoani humo.

Akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa ofisi ya mkuu wa wilaya ya kiteto mwenyekiti wa kamati ya ujenzi huo Faraja Ngerageza amesema mradi huo umeanza mwaka 2023 na unatarajia kuanza kutumika mwezi march mwaka huu.
Baadhi ya wananchi wa Kiteto wamemshukuru Waziri mkuu kwa kufika na kusikiliza pamoja na kutatua kero za wananachi.
Aidha, waziri mkuu anaendelea na ziara yake mkoani Manyara ambapo kwa Sasa yupo wilayani Simanjiro na kuzindua mradi pamoja na kusikiliza na kutatua kero za wananachi.