FM Manyara
FM Manyara
23/02/2026, 22:26

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga amewaagiza Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini(TARURA) na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROAD) Mkoa wa Manyara kuomba fedha za dharura kukarabati barabara zinazoharibiwa na mvua.
Na Mzidalfa Zaid
Amesema hayo Leo katika kikao Cha bodi ya barabara mkoa wa Manyara kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Manyara.
Amesema amepata taarifa ya baadhi ya barabara ambazo zimeharibiwa na mvua ikiwemo barabara ya Bashnet-Orbesh.

Kwa upande wake meneja wa wakala wa barabara (TANROAD) mkoa wa Manyara Dutu Masele , amesema changamoto ya mashimo katika barabara ya Katesh – Singida imesababishwa na magari ya mizigo mizito kuongezeka ambapo kwa Sasa magari 650 hupita mkoani Manyara hali inayopelekea barabara kushindwa kuhimili.

Aidha meneja wa wakala wa barabara za vijijini na mijini (TARURA) mkoa wa Manyara Injinia Salim Bwaya amesema wanaendelea kukarabati barabara za mkoa wa Manyara ikiwemo barabara ya kutoka Babati kuelekea ikulu.

