FM Manyara

Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Babati lajadili rasmi ya mpango na bajeti kwa mwaka fedha 2026/2027

17 February 2026, 5:44 pm

picha ya mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Babati John Noya pamoja na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Babati Anna Mbogo

Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Babati limejadili rasmi ya mpango na bajeti kwa mwaka fedha 2026/2027 na kugusa sekta mbali  mbali.

Na Mzidalfa Zaid

Katika baraza hilo mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Babati John Noya amewataka madiwani kuhakikisha wanasimamia miradi iliyoko kwenye kata zao kwa kuwa ni wawakilishi wa wananchi.

Noya amesema bajeti ya  vituo vyote vya afya katika halmashauri ya wilaya ya Babati ni zaidi ya shilini millioni 655.

sauti ya mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Babati John Noya

kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Babati Anna Mbogo amewataka madiwani kufanya uhamasishaji wa makusanyo ya mapato ya ndani. 

Sauti ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Babati Anna Mbogo

Awali baadhi ya madiwani wamelalamikia changamoto ya magari kutopita maeneo ya stendi ikiwemo stendi ya Dareda na kupelekea kupoteza mapato ya ndani.

sauti ya baadhi ya madiwani
picha ya baadhi ya madiwani