FM Manyara

Halmashauri ya wilaya ya Babati kunufaika na elimu ya uhifadhi

16 February 2026, 5:16 pm

Picha ya uzinduzi

Shirika la Lesson in Conservation (L.I.C) kwa kushirikiana na Taasisi ya Chem Chem Association wamezindua mradi wa elimu ya uhifadhi mashuleni unaolenga shule za msingi na sekondari zilizopo  katika kata tatu zinazunguka hifadhi ya Tarangire na Manyara.

Na Marino Kawishe

Akizungumza na maafisa elimu kata  na wakuu wa idara mbali mbali kutoka halmashauri ya wilaya ya Babati mwakilishi wa shirika hilo GloriaTarimo amesema mradi huo utawafikia jumla ya watoto elfu tano kutoka shule za msingi na sekondari zitakazofikia 21, kutoka kata ya Nkaiti, Mwada na Magara  ambao  utatekelezwa kwa miaka mitano.

sauti ya mwakilishi wa shirika hilo GloriaTarimo

Kwa upande wake  mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Babati Anna Mbogo amesema mradi huo unapaswa kutoa elimu  kwa wanafunzi wa shule hizo kwa manufaa ya kizazi cha leo na baadae huku akizitaka idara za elimu na mali asili  kuingiza  kwenye mipango yao masuala yanayohusu uhifadhi.

Sauti ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Babati Anna Mbogo

Nae mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Chem Chem Association  Clever Zulu amesema lengo la Taasisi hiyo ni kujenga jumuiya ya mfano Africa kupitia uhifadhi wa jamii chini ya jumuiya ya Burunge WMA na wananchi kwenda  kujifunza  namna bora ya uhifadhi kwenye maeneo yao.

Sauti ya mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Chem Chem Association  Clever Zulu

Aidha,mradi huo pamoja na mambo mengine utawapa fursa wanafunzi kutembelea maeneo ya hifadhi hapa nchini na kujifunza kwa vitendo faida za uhifadhi na ukitarajiwa  kugharimu zaidi ya shilingi milioni 156 mpaka kukamilika kwake.