FM Manyara

RC Sendiga  akabidhi  kadi  za bima ya afya kwa wote  kwa  kaya maskini

7 February 2026, 11:01 am

Picha ya Mkuu wa mkoa wa Mnyara  Queen Sendiga Akikabidhi kadi za bima afya kwa wananchi

Zaidi  kaya  maskini 60 katika kijiji cha Imbilili wameanza kunufaika na mpango wa bima wa afya kwa wote  katika mpango wa kwanza wa ugawaji wa bima hizo.

Na Emmy Peter

Akikabidhi kadi hizo  kwa wananchi hao mkuu wa mkoa wa Mnyara  Queen Sendiga  amesema kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa hadi za Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr.Samia Suluhu Hasani katika siku 100 za uongozi wake ambapo amesema  kila mwananchi anatakiwa kupata  bima ya afya na katika mkoa wa Manyara zoezi hilo linaendelea  kuwafikia wananchi katika maeneo yao.

sauti ya mkuu wa mkoa wa Manyara  Queen Sendiga 

Aidha mwenyekiti wa kijiji cha Imbilili Marisel Visent  ameishukuru serikali ya awamu ya sita  kwa kuwakumbuka wananchi wa kaya masikini ambapo amesema ni msaada mkubwa  kwa  wananchi hao 

sauti ya kijiji cha Imbilili Marisel Visent 

Sambamba na hilo amewataka wananchi  kuendelea kutunza bima hizo ili kuwanufaisha   katika matibabu.