FM Manyara

REA kusambaza umeme vitongoji 267 Manyara

6 February 2026, 4:57 pm

picha ya mwakilishi  wa mkurugenzi mkuu wa REA, Mhandisi Herini Mhina na Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga

Serikali  imeanza  utekelezaji  wa mradi  wa kusambaza umeme  katika vitongoji  267 vya mkoa wa Manyara  kwa gharama ya shilingi bilioni 45.8 kupitia wakala wa nishati vijijini (REA).

Na Mzidalfa Zaid

Akizungumza  wakati wa  kumtambulisha  mkandarasi, mwakilishi  wa mkurugenzi mkuu wa REA, Mhandisi Herini Mhina, amesema mkataba wa utekelezaji mradi huo ni wa miaka 3 katika halmashauri zote za mkoa wa Manyara.

sauti ya mwakilishi  wa mkurugenzi mkuu wa REA, Mhandisi Herini Mhina

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga, amewaagiza wakuu wa wilaya zote  za mkoa wa Manyara kutoa  ushirikiano  kwa mkandarasi  huyo na  kutoa elimu kwa wananchi kuwa mradio huo hauna fidia.

sauti ya mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga

Aidha, mkandarasi mkandarasi ambae amekabidhiwa mradi huo Patrick Mong, amesema  Wana Lengo la kukamilisha mradi huo kwa miezi 33 na wanaanza kazi  February 9 mwaka huu.

sauti ya mkandarasi mkandarasi ambae amekabidhiwa mradi huo Patrick Mong