FM Manyara
FM Manyara
5 February 2026, 7:08 pm

Moafisa Mawasiliano wa serikali kutoka halmashauri saba za mkoa wa Manyara wametembelea kujionea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Stendi mpya ya kisasa ya mabasi ya Babati mjini na kuvutiwa na wingi wa wanawake wanaoshiriki kazi za ujenzi kuanzia kichimba msingi wa majengo mbalimbali katika mradi huo unaotekelezwa na serikali kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 5.6.
Na Mzidalfa Zaid
Afisa habari wa mkoa wa Manyara Ruth Kyelula na afisa habari wa wilaya ya Hanang Carol Gismoy wamewapongeza wanawake hao kwa moyo wao wa uthubuto kushiriki shughuli za ujenzi ambazo mara nyingi hufanywa na wanaume na kwamba hiyo inaondoa ile dhana ya kubagua kazi kwa mrengo wa jinsia.
Kwa mujibu wa msimamizi wa mradi huo wa ujenzi, handisi Innocent Mandago, mradi huo amesema ulioanza Oktoba mwaka jana, mradio huo unatoa kipaumbele kwa wenyeji wa mkoa wa Manyara na hasa wanawake kufanya shughuli za ujenzi wa hatua mbalimbali ili waweze kujipatia mapato ya kijikimu na kunufaika na mradi huo katika hatua hiyo ya ujenzi.
Mkandarasi msimamizi, mhandisi John Bhoke anasema wanawake ni kati ya wafanyakazi takribani 100 wanaofanya kazi za kila siku katika mradi huo kuanzia kuchimba mtaro, kujenga msingi wa majengo, kukoroga zege na shughuli zingine ili kujipatia kipato.
Baadhi ya wanufaika wa mradi huo Mary Safari na Getruda Gabriel wameshukuru serikali kuwaletea mradi huo na kwamba wanajiona fahari kuwa sehemu ya mradi huo kwani wanajipatia kipato cha kuhudumia familia zao.
Maafisa Mawasiliano hao wamefanya ziara hiyo baada ya kikao kazi cha siku mbili mjini Babati kujikimbusha majukumu yao ya kila siku ya kutangaza shughuli za serikali ikiwemo miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali katika maeneo yao.