FM Manyara
FM Manyara
26 January 2026, 10:31 pm

Mamia ya wananchi wamejitokeza kupata huduma ya mifupa,pua sikio,koo na macho katika hospital ya rufaa ya mkoa wa Manyara .
Na Mzidalfa Zaid
Hatua hii imekuja baada ya Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Manyara kwa kushirikiana na hospital ya rufaa Kanda ya Mbeya pamoja na Shirika la KCCO kuandaa kambi ya madaktari bingwa maalumu wa mifupa ,pua, sikio,koo na macho ambayo imeanza Leo January 26 Hadi January 30 mwaka huu wa kwa lengo la kuwapatia Wateja huduma za kibingwa.
Baadhi ya wagonjwa ambao wamejitokeza kupatiwa matibabu wamesema wamepata huduma nzuri ya matibabu ambapo wameipongeza hatua hiyo kwani walikuwa wakifuata huduma hizo mbali na kuingia gharama kubwa.
Kwa upande wake kaimu mganga mfawidhi hospital ya rufaa mkoa wa Manyara Dokta Yesige Mutajwaa Amesema kwa siku ya Leo ya kwanza Zaidi ya wagonjwa 200 wamefika kupatiwa matibabu.

Nae daktari bingwa wa mifupa kutoka hospital ya rufaa Kanda ya Mbeya Dokta Baraka Mponda amesema kwa siku ya Leo wamewahudumia wananachi wengi wenye matatizo ya mifupa .
Meneja mradi wa shirika la KCCO Manyara Patricia Malley ambao wamedhamini kambi hiyo, wamesema Lengo la kudhamini ni kuhakikisha wananachi wanapatiwa matiababu ya uhakika.