FM Manyara
FM Manyara
22 January 2026, 7:10 pm

Wizara ya afya chini ya Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Manyara kwa kushirikiana na hospital ya rufaa Kanda ya Mbeya pamoja na shirika la KCCO wameandaa kambi ya madaktari bingwa maalumu wa mifupa ,pua, sikio,koo na macho itakayofanyika mkoani Manyara kuanzia January 26 mpaka 30 mwaka huu wa 2026 kwa lengo lakuwapatia Wateja huduma za kibingwa.
Na Mzidalfa Zaid
Akizungumza na Fm Manyara Afisa muuguzi msaidizi kutoka Kitengo cha Macho hospitali ya Rufaa mkoa wa Manyara Faraja Mapunda amesema huduma zitakazotolewa ni pamoja na uchunguzi na matibabu ya mifupa, pua, sikio,koo,macho

Kwa upande wake Afisa Muuguzi msaidizi kutoka hospitali ya Rufaa mkoa wa Manyara Macrina Kilamba ameelezea faida za kambi hiyo ya siku tano na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupima afya zao.
