FM Manyara
FM Manyara
16 January 2026, 9:00 pm

Mamlaka za maji ikiwemo Ruwasa, Bawasa na waatalam kutoka Maabara za maji mkoa wa Manyara na bonde la maj na bonde la kati zimekutana kwa pamoja na kuunda timu kwa ajili ya kuweka mipango ya upatikanaji wa maji ili ifikapo mwaka 2030 mkoa wa Manyara unakuwa na maji kwa asilimia 99.
Na Mzidalfa Zaid
Akiongea baada ya kikao hicho Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Babati(BAWASA) Iddi Msuya amesema wameweka mkakati wa kuhakikisha wanashirikiana kufanikisha upatikanaji wa maji mjini na vijijini.
Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira vijijini(RUWASA) Injinia James Kionaumela, amesema mashirikiano hayo yatasaidia kupunguza changamoto mbalimbali ikiwemo kuazimana vifaa.
Mkuu wa Maabara ya maji mkoa wa Manyara Nikolaus Germanus, amesema hali ya ubora wa maji katika mkoa wa Manyara inaridhisha.
Nae Mhandisi wa maji kutoka Bonde la maji, bonde la kati katika ofisi ya Babati Denis Gunze, amesema wameweka mikakati ya kuhakisha wanafanya utafiti juu ya upatikanaji wa maji sehemu yenye maji.