FM Manyara
FM Manyara
16 January 2026, 9:03 pm

Mkuu wa mkoa wa manyara Queen Sendiga amewataka wazazi na walezi mkoani Manyara kuhakikisha wanawapeleka shule watoto ambao wanatakiwa kwenda shule kwakuwa bado wapo wanafunzi ambao hawajaripoti.
Na Mzidalfa Zaid
Amesema hayo leo wakati akiongea na waandishi wa habari ofisni kwake, amesema mpaka sasa wanafunzi wachache wa kidato cha kwanza wameripoti hivyo viongozi wa kata na vijiji wanaendelea na misako ya kuwatafuta wanafunzi ambao hawajaripoti.
Aidha, amewataka wazazi na walezi mkoani hapa kuchangia chakula mashuleni ili watoto wapate haki yao ya msingi ya kupata lishe bora na masomo.