FM Manyara
FM Manyara
13 January 2026, 7:01 pm

Mamlaka ya dawa na vifaa tiba TMDA Kanda ya kaskazini imetoa elimu kwa wananchi mkoani Manyara na kanda ya kaskazini kwa ujumla namna ya kuhifadhi dawa ili zisipoteza uwezo wa kufanya kazi.
Na Mzidalfa Zaid
Elimu hiyo imetolewa na Meneja wa Mamlaka ya dawa na vifaa tiba TMDA Kanda ya kaskazini Proches Patrick wakati akiongea na fm Manyara, amesema dawa hazipaswi kuhifadhiwa sehemu ambayo ina maji, au joto kali.
Aidha, amewataka wananchi wa Kanda ya kaskazini kwa ujumla kuzingatia matumizi sahihi ya dawa kama wanavyoshauriwa na daktari.