FM Manyara
FM Manyara
8 January 2026, 7:39 pm

Mbunge wa jimbo la Babati Mjini Mhe Emmanuel Khambay amehaidi kusaidia wananchi wa jimbo hilo kupata Kituo cha kudurufu mitihani ya majaribio kwa wanafunzi wanaosoma sekondari ili kupandisha ufaulu wao kwa shule za serikali zilizopo jimboni kwake.
Na Marino Kawishe
Akizungumza na wananchi wa Kata ya Nangara, amesema mpango huo utakuwa ni wakuboresha eneo la ufaulu kwa wanafunzi ili waendenane na shule za binafsi ambazo zimekuwa zikifanya vizuri ambapo ameshauri mitihani hiyo iwe inafanyika kila mwezi.

Kwenye ziara hiyo Mh Khambay ameambatana na baadhi ya wataalamu kutoka ofisi ya halmashauri ya mji wa Babati waliojibu kero zilizoulizwa na wananchi moja kwa moja huku akiwata kuendelea kushirikiana na wananchi kuleta maendelo na kuacha kusuasua na kuwapatia wananchi huduma wanazostahili bila upendeleo.