FM Manyara
FM Manyara
8 January 2026, 7:26 pm

Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga ametoa wito kwa wafanyabiashara wa mkoa huo kutumia fursa za kibiashara zinazojitokeza ndani na nje ya mkoa huo.
Na Mzidalfa Zaid
Sendiga ametoa wito huo wakati alipokuwa kwenye maonesho ya 12 ya kimataifa ya biashara zanzibar kwenye banda maalumu la mkoa wa Manyara ambapo washiriki mbalimbali kutoka katika halmashauri zote za mkoa huo walipata nafasi ya kutangaza bidhaa zao kupitia maonesho yao.
Akiwa kwenye banda maalum la mkoa wa Manyara Sendiga amesema lengo ni kufanyabiashara,kujifunza, kuutangaza mkoa wa Manyara, kutangaza bidhaa zilizopo mkoani humo pamoja na kuwaunganisha wafanyabiashara wa mkoa huo na wafanyabiashara wengine .
Aidha, Sendiga amesema wao kama mkoa ni mara ya kwanza kushiriki maonesho hayo,hivyo amepata fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali kujionea bidhaa tofauti na zile zilizopo mkoa wa manyara