FM Manyara
FM Manyara
7 January 2026, 5:17 pm

Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga, amewataka wazazi na walezi mkoani Manyara kuhakikisha wanawapeleka watoto shule mwanzoni mwa mwaka huu wa masomo nakusema wazazi wanapaswa kutoa ushirikiano kwa walimu kuhusu utoaji wa chakula mashuleni.
Na Emmy Peter
Sendiga ameyasema hayo katika kijiji cha Chem chem kata ya Mutuka ambapo amewataka makatibu Tawala, na Watendaji wa kata hiyo pamoja na maafisa elimu kata kuhakikisha malengo ya mkoa yaliyowekwa yanatimia kwa kuhakikisha wanafunzi wanaingia shule kwa wakati.
Aidha, Sendiga amesema serikali itaandaa sheria zitakazowabana wazazi wasiotimiza wajibu huo kwa watoto wao kuwapeleka shule kwakua ni maelekezo ya serikali.