FM Manyara
FM Manyara
7 January 2026, 4:48 pm

Serikali mkoani Manyara imewataka wananachi mkoani Manyara kutovamia maeneo yaliyotengwa na serikali kwa ajili ya shughuli maalum ili kuepuka migogoro ambayo imekuwa ikitokea.
Na Mzidalfa Zaid
Wito huo umetolewa leo na Kamishna wa ardhi mkoa wa Manyara Wensilaus Mtui wakati akiongea na fm Manyara, amewaonya wananachi wenye tabia hiyo ya kuvamia maeneo ya serikali na kufanya shughuli zao za kiuchumi.
Aidha,amewataka wananachi kufuata sheria za umiliki wa ardhi kwa kuhakikisha maeneno yao yanapimwa na kumilikiwa ili kusitokee mgongano wa kiwanja kimoja kumilikiwa na watu zaidi ya mmoja .