FM Manyara

Serikali kuweka mazingira rafiki ya elimu

6 January 2026, 5:37 pm

Picha ya nyumba za walimu

Mkuu wa mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, amesema serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo pamoja na wananchi ili kuboresha mazingira ya elimu nchini, kwa lengo la kuhakikisha watoto wote wanapata elimu bora, salama na yenye viwango vinavyokubalika.

Na Emmy Peter

Sendiga ameyasema hayo  wakati wa uzinduzi wa nyumba mbili za walimu katika shule ya msingi Chem chem, iliyopo katika  kata ya Mutuka, wilaya ya Babati,  mkoani Manyara, amesema hatua hiyo inalenga kuwavutia walimu kufanya kazi katika mazingira rafiki na na kuongeza ufanisi katika utoaji wa elimu kwa wanafunzi.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga

Aidha, mradi wa ujenzi wa nyumba hizo umetekelezwa na serikali kwa kushirikiana na wananchi pamoja na wadau wa maendeleo Mikuyu Tanzania na Impact Lead Tanzania ambapo umegharimu zaidi ya shilingi milioni 195 hadi kukamilika kwake.

Kwa upande wake mwakilishi wa kampuni ya Mikuyu  amesema katika mradi huo wa nyumba 2 za walimu , wadau wameshiriki kuunga mkono  jitihada za kumalizika kwa mradi ambapo amesema wanaendelea kufanya maboresho mbalimbali shuleni hapo.

Sauti ya mwakilishi wa kampuni ya Mikuyu