FM Manyara
FM Manyara
5 January 2026, 5:28 pm

Wananchi mkoani Manyara wameshauriwa kuendelea kufuatilia ushauri unaotolewa na Mamlaka hiyo ili kuwasaidia katika shughuli zao.
Na Mzidalfa Zaid
Meneja wa Mamlaka ya Hali ya Hewa mkoa wa Manyara Salma Amour ameyasema hayo leo wakati akiongea na FM Manyara, amesema kwa mwezi Januari vipindi vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache ambapo amesema kuanzia Januari 5 hadi 10 vipindi vya mvua chache vinatarajiwa katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Manyara.
Aidha, amewashauri wakulima, wafugaji pamoja na wavuvi kufuatilia utabiri unaotolewa na TMA ili kurahisisha shughuli zao zao kila siku.