FM Manyara
FM Manyara
22 December 2025, 9:22 pm

Waajiri mkoani Manyara wametakiwa kulipa michango ya wafanyakazi kwa wakati pamoja na kuwaandikisha wafanyakazi wote ambao hawajandikishwa katika mfuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii(NSSF) ili wanufaike na fursa mbalimbali zinazopatikana katika mfuko huo.
Na Mzidalfa Zaid
Hayo yameelezwa leo na Meneja wa NSSF mkoa wa Manyara Alexanda Joseph wakati akiongea na fm Manyara, amesema kumekuwepo na changamoto ya baadhi ya waajiri ambao wamekuwa wakilipa michango midogo tofauti na mishahara ambayo wafanyakazi wanapokea, ambapo amekemea vitendo hivyo.
Aidha, amewataka wafanyakazi wote ambao wamekuwa wakifanya kazi bili kupeleka michango NSSF wafike kwenye ofisi za NSSF Manyara ili hatua zaidi za kisheria zichukuliwe na wafanyakazi hao wapate haki zao.