FM Manyara
FM Manyara
19 December 2025, 7:37 pm

Mpango wa uhamasishaji wa Bima ya afya kwa wote umezinduliwa katika katika mkoa wa Manyara utakao saidia wananchi wa mkoa wa Manyara kupata huduma za matibabu kwa urahisi na unafuu.
Na Emmy Peter
Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amezindua mpango wa uhamasishaji wa utekelezaji wa Bima ya afya kwa wote ambapo mpango huo umezinduliwa katika halmashauri ya mji wa Babati na utasaidia kupunguza gharama za matibabu kwa wananchi wa mkoa wa Manyara..
Sendiga amezindua mpango huo leo katika ukumbi wa chuo kikuu Huria mjini Babati, amesema mpango huo wa Bima ya afya NHIF kwa wote utasaidia wananchi wa mkoa wa Manyara kupata huduma za matibabu kwa urahisi na unafuuu na wananchi watapatiwa elimu kuhusu umuhimu wa Bima ya afya kwa mtu mmoja mmoja itakayosaidia katika matibabu.
Kwa upande wake mganga mkuu wa mkoa wa Manyara Dokta Andrew Method amesema kwa mkoa wa Manyara imekuwa ni fursa katika kuendelea kuboresha huduma za afya kwa wananchi katika Halmashauri zote 7 ndani ya mkoa wa Manyara na wamejipanga kupeleka elimu hiyo katika makundi mbali mbali.
Aidha watumishi wa afya wa mkoa wa Manyara wameishukuru serikali ya awamu ya sita kuleta huduma hiyo ya Bima ya afya kwa wote kwakua itasaidia kuleta unafu katika kazi zao na kuondoka na msamahaa wa wagonjwa wanao shindwa kulipia huduma hizo za matibabu.