FM Manyara
FM Manyara
19 December 2025, 10:14 am

Zaidi ya shilingi milion 150 zimetumika kukamilisha ujenzi wa zahanati ya Endagile iliyopo kata ya Mamire wilayani Babati mkoani Manyara ambapo wananchi wa kijiji hicho wamechangia fedha na nguvu kazi huku pia wadau na mbunge wa jimbo la Babati vijijini kuchangia kukamilika kwa majengo hayo.
Na Marino Kawishe
Akizungumza mbele ya wananchi wa kijiji hicho mgeni rasmi ambae ni mkurugenzi wa halmashauri ya wilayani ya Babati Anna Mbogo amesema baada yakukamilika kwa zahanati hiyo inatoa fursa kwa wananchi wa kijiji hicho na jirani kupata matibabu mbali mbali na kuondokana na umbali mrefu uliokuwepo hapo awali.

Kwa upande wake mganga mkuu wa hospital ya wilaya ya Babati Dr Madama Hosea amesema huduma zinaanza kutolewa mara moja baada ya kukamilika kwa majengo ya zahanati hiyo huku akitaja baadhi ya huduma zitakazoanza kutolewa kuanzia dec 19.
Naye mratibu wa vituo vya taarifa na maarifa mkoani Manyara Clara Malley amesema wao kama wanakikundi mnamo mwaka 2022 walitoa pendekezo kwa mkurugenzi wa halmashauri kujengwa zahanati na miundo mbinu mingine itakayosaidia wananchi hasa wakati wa mvua.
Wakionge na Fm Manyara redio wananchi wa kijiji hicho wamekiri uwepo wa zahanati hiyo , ambapo wamesema itawasaidia kupata huduma ikiwemo clinic kwa wajawazito na huduma nyingine zitakazotolewa na wataalamu wa afya.
