FM Manyara

NIDA yawataka Wananchi Manyara kusahihisha taarifa zao

18 December 2025, 4:56 pm

Picha ya mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) mkoa wa Manyara Amwesiga

Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kufika katika ofisi za Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) ili kufanya mabadiliko na kusahihisha taarifa zao za awali ambazo sio sahihi katika Vitambulisho vyao vya taifa NIDA.

Na Mzidalfa Zaid

Wito huo umetolewa leo na afisa usajili wa mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) mkoa wa Manyara Amwesiga Bandio alipozungumza na Fm Manyara amesema mkurugenzi mkuu wa NIDA ametangaza kibali cha mwaka mmoja kwa wale wote ambao walikuwa hawakidhi kigezo cha kufanya mabadiliko ikiwa ni pamoja na kughushi nyaraka na kutoa taarifa ambazo sio sahihi.

sauti ya afisa usajili wa mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) mkoa wa Manyara Amwesiga Bandio alipozungumza na Fm Manyara

Aidha Bandio amesema muitikio wa watu wanaofika kujisajili ni mkubwa na kuwataka watu wengine ambao bado hawajapata vitambulisho hivyo wafike katika ofisi zao ili kujisajili na badae kupata vitambulisho vyao kwani vina umuhimu mkubwa na vinatumika katika sehemu mbalimbali.