FM Manyara

Wafanyabiashara  Manyara washauriwa kuwa na mpango mkakati

16 December 2025, 8:15 pm

picha ya viongozi wa TNCC Manyara

Wafanyabiashara mkoani  Manyara wametakiwa kuzingatia vigezo, sheria na matakwa yote ya kibiashara  ili kuepuka kupata adhabu mbalimbali ambazo wanawaweza kuzipata na kupelekea kushuka kibiashara.

Na Mzidalfa Zaid

Wito huo umetolewa leo na Meneja wa Chemba ya Taifa ya biashara (TNCC) mkoa wa Manyara Zainab Rajabu , amesema katika kipindi hiki cha sikukuu wafanyabiashara wanapaswa kuzingatia ubora na huduma nzuri kwenye biashara zao.

Amesema wamekuwa wakitoa ushauri kwa wafanyabiashara hivyo wafanyabiashara wanapojiunga na TNCC wanapata fursa ya kupewa elimu pamoja na kuunganishiwa masoko.

sauti ya Meneja wa Chemba ya Taifa ya biashara (TNCC) mkoa wa Manyara Zainab Rajabu

Kwa upande wake afisa mshauri wa maendeleo ya biashara TNCC mkoa wa Manyara Lairumbe Laizer, amewataka wafanyabiashara kuwa na  mpango mkakati katika biashara zao ili kukuza uchumi kupitia biashara hizo.

sauti ya afisa mshauri wa maendeleo ya biashara TNCC mkoa wa Manyara Lairumbe Laizer