FM Manyara
FM Manyara
16 December 2025, 5:47 pm

Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amezindua clinik ya madaktari bingwa ya magonjwa ya binadamu katika halmashauri ya mji Mbulu ili kuwasaidia wananchi kupunguza kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya za kibingwa
Na Emmy Peter
Sendiga amezindua kliniki hiyo ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake katika mkoa wa Manyara ambapo amesema tangu kuanzaa kwa zoezi la huduma hiyo ya clinik za madaktari bingwa wamesha hudumia zaidi ya wagonjwa 2174 na huduma hiyo imesaidia wananchi kupata huduma kwa haraka.
Kwa upande wao wananchi wameishukuru serikali ya awamu ya 6 kwa kuwasogezea huduma hizo karibu kwakua huduma hiyo walikuwa wakiifata nje ya mkoa wa Manyara.