FM Manyara
FM Manyara
15 December 2025, 4:46 pm

Wananchi mkoani Manyara wameshauriwa kufuatilia taarifa zinazotolewa na Mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA)pamoja na kuwasiliana na maafisa ugani wa maeneo yao ili wajue mbegu zinazofaa kupanda na kulima kwa kuhifadhi maji wakati huu wa msimu wa mvua chache .
Na Mzidalfa Zaid
Hayo yamesemwa na Meneja wa TMA mkoa wa Manyara Salma Amour alipokuwa akizungumza na fm Manyara amesema kwa mkoa wa Manyara mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi chini ya wastani kwa msimu huu wa mvua za mwezi december.
Aidha Amour amewataka wananchi kuchukua tahadhari za mapema ikiwemo kuhifadhi chakula cha kutosha kwaajili ya matumizi yao ya badae pamoja na chakula cha mifugo.