FM Manyara
FM Manyara
13 December 2025, 11:27 am

Madereva kote nchini wametakiwa kuacha tabia ya kuendesha vyombo vya Moto pindi wanapotumia vilevi kwakua itasaidia kupunguza ajali za barabarani msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.
Na Emmy Peter
Kamishina msaidizi wa Polisi (ACP) Joseph Mwakabonga kutoka kikosi cha usalama barabarani nchini ameyasema hayo alipokuwa katika ziara yake ya ukaguzi wa mabasi ya safari za usiku mkoani Manyara, amesema wameanza zoezi la ukaguzi wa magari hayo na kubani baadhi ya makosa.
Mwakabonga amesema Katika kipind hiki Cha sikukuu wamebaini kuna makosa ambayo madereva wanayafanya kwa kuendesha magari kwa mwendo kasi bila kuchukua tahadhari ambapo amewataka kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.
Aidha, Mwakabonga Amesema Katika zoezi hilo la ukaguzi wa magari wamejipanga kuhakikisha madereva wote wanakuwa na leseni na zoezi hilo ni endelevu ambapo linafanyika usiku na mchana