FM Manyara
FM Manyara
8 December 2025, 5:11 pm

Wamiliki wa magari ya shule mkoani Manyara wametakiwa kusimamia magari ya kubeba wanafunzi na kuhakikisha magari hayo ni mazima ili kuondokana na ajali zinazo sababishwa na magari mabovu.
Mkuu wa kikosi cha usalama bara barani mkoa wa Manyara Michael Mwakasungula, ameyasema hayo alipokuwa katika zoezi la ukaguzi wa magari ya shule amesema mwitikio kwa wamiliki wa magari ya shule ni mkubwa na wanaendelea kujitokeza kupeleka magari yao kukaguliwa na kubaini changamoto za magari hayo ya kubebea wanafunzi.
Kwa upande wake mkaguzi wa magari wilaya ya Babati sajent Mohamed Yahaya amesema katika ukaguzi huo uliyo fanyika wamekagua ufanyaji wa kazi wa mifumo yote ya magari ya shule na kubaini baadhi ya changamoto katika magari hayo ambapo wamewataka wamiliki kuwa na utaratibu wakupeleka magari hayo kukaguliwa mara kwa mara.