FM Manyara
FM Manyara
3 December 2025, 5:47 pm

Mkuu wa mkoa wa manyara, Queen Sendiga, anatarajia kuanza ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi pamoja na kutemblea miradi mbalimbali na ziara hiyo itafanyika chini ya kampeni maalum iitwayo “tunavua buti ama hatuvui, tukutane saiti”, ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya awali ya “sivui buti mpaka kieleweke.”
Na Mzidalfa Zaid
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Sendiga amesema ziara hiyo itaanza disemba 4, 2025, ikiwa na lengo la kukagua miradi katika sekta mbalimbali, kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Aidha, amesema ziara hiyo itafanyika katika kata zote 142 za mkoa wa manyara, na kusema kuwa atahakikisha changamoto zote zinatatuliwa , huku akiwataka wataka watendaji kuandaa taarifa kamili ili wawe na majibu ya kutosha watakapo ulizwa taarifa yeyote.